December 31, 2025
Pre Internship Examination for Medical, Dental and Allied Health Students who are expecting to do...
Read moreDecember 31, 2025
For those Medical, Dental and Allied Health practitioners who completed their internship training shall be...
Read moreTANGAZO KWA WATARAJALI WALIOSALIA KUPATA BARUA KWA INGIZO LA MWEZI NOVEMBA 2026
Baraza la Madaktari Tanganyika linawatangazia watarajali ambao hawajapata barua za utarajali kwa awamu ya Novemba 2026 kuwa mfumo utafunguliwa tena kwa ajili ya kuomba vituo vya mafunzo vyenye nafasi. Zoezi hili linawahusu watarajali ambao hawakufanikiwa kupata vituo kutokana na vituo walivyoomba kuwa vimejaa, na hivyo hali ya maombi yao kwenye mfumo kusomeka “Unattended”. Watarajali hao watapata fursa ya kuomba vituo vya mafunzo ambavyo bado vina nafasi.
Mfumo utafunguliwa leo, tarehe 25 Novemba 2026, kuanzia saa 12:00 jioni hadi tarehe 26 Novemba 2026, saa 6:00 usiku.
Watarajali wanapaswa kuzingatia kuwa mfumo utaonyesha vituo vya mafunzo vyenye nafasi pekee. Hivyo, endapo kituo hakionekani kwenye mfumo, ina maana kuwa nafasi za mafunzo katika kituo hicho zimejaa.
Baada ya kuchagua kituo kupatiwa usajili wa muda (Provisional Registration), watarajali watatakiwa kuchapisha vyeti vya usajili wa muda pamoja na barua za upangaji wa vituo (Appointment Letters) kupitia mfumo na kuripoti katika vituo walivyopangiwa kwa ajili ya kuanza mafunzo ya utarajali.
Imetolewa na:
MSAJILI BARAZA LA MADAKTARI TANGANYIKA
25 Novemba 2026
| Title: | Adapted etat course for pediatric emergency medicine on district level |
| Provider: | Sengerema Designated District Hospital |
| Location: | Sengerema Designated District Hospital |